Swalah 100.000 ni Makkah yote au ni msikiti mtakatifu tu?


Swali: Swalah moja ambayo ni sawa na swalah 100.000 ni Haram yote au ni kwenye Msikiti Mtakatifu peke yake?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba ni Haram yote; vyote vilivyoko kwenye mpaka wa Haram vinaitwa “msikiti Mtakatifu”. Hata hivyo lililo bora zaidi ni kuswali karibu na Ka´bah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018