Katika mwezi huu tunapasa kutoa swadaqah kwa wingi. Kuna swadaqah sampuli mbili:

1 – Swadaqah ya wajibu. Nayo ni ile zakaah.

2 – Swadaqah iliyopendekeza. Nayo ni ile swaqadaqah ya mtu kujitolea mwenyewe.

Kwa hivyo toa swadaqah kwa wingi ndani ya mwezi huu kuwapa mafukara, masikini na wale watu wenye madeni na wengineo katika wahitaji. Kwani hakika swadaqah ndani ya mwezi huu ina sifa maalum ukilinganisha na miezi mingine.

Kuhusu zakaah ni swadaqah ya lazima. Nayo ni bora kuliko swadaqah iliyopendekezwa ya kujitolea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika yale aliyopokea kutoka kwa Mola (´Azza wa Jall) ambaye amesema:

”Mja Wangu hatojikurubisha kwa chochote ninachokipenda zaidi kuliko yale niliyomfaradhishia.”[1]

Kwa ajili hii baadhi ya wanadhani kuwa mambo yaliyopendekezwa ni bora kuliko mambo ya faradhi. Mambo sivyo kabisa. Bali mambo ya faradhi ni bora kuliko yale mambo yaliyopendekezwa kutokana na Hadiyth hii. Endapo yangelikuwa si bora na yenye kupendeza zaidi mbele ya Allaah basi asingewafaradhishia nayo waja.

[1] al-Bukhaariy (6502).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/202)
  • Imechapishwa: 06/04/2022