Suufiyyah wasiokuwa na chembe ya Tawhiyd

Swali: Waabudu makaburi na wale Suufiyyah waliopindukia wana shirki na Tawhiyd?

Jibu: Hapana. Yule anayeabudu makaburi hana Tawhiyd. Tawhiyd haiwezi kukusanyika na shirki. Yule anayeabudu makaburi kwa maana ya kwamba anamuomba yule mfu aliyemo ndani ya kaburi, anamchinjia au anamuwekea nadhiri ni mshirikina. Ikipatikana shirki kubwa Tawhiyd inapotea kama ambavyo ikipatikana Tawhiyd shirki nayo inapotea. Haviwezi kukusanyika. Shirki kubwa haiwezi kukusanyika pamoja na Tawhiyd. Hilo kamwe. Ikipatikana shirki kubwa Tawhiyd inapotea kama ambavyo ikipatikana Tawhiyd shirki kubwa inapotea. Vivyo hivyo unafiki mkubwa na kufuru kubwa. Lakini shirki ndogo na maasi vinaweza kukusanyika na Tawhiyd. Lakini pamoja na shirki kubwa ni jambo lisilowezekana.

Suufiyyah wanatofautiana. Kuna ambao wanaweza kuwa na Bid´ah iliyochanganyikana na Tawhiyd. Hao ni baadhi ya wale wenye kuipa nyongo dunia. Kuhusu Suufiyyah ambayo imefikia katika kiwango cha kufuru haiweiz kukusanyika pamoja na Tawhiyd. Mfano wa wale Suufiyyah wenye kuamini kila kiumbe ni Allaah, wale wanaotumbukia katika shirki kubwa au wanashirikisha katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hawa hawawezi kuwa na chembe ya Tawhiyd.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67941&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 29/07/2017