Mwenye kuonelea kuwa mtu maalum au watu wote kwa jumla wanaweza kupita njia nyingine mbali na ile njia iliyopitwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkufuru Allaah na Mtume Wake. Kama mfano wa wale wenye kudai kwamba wako mawalii wake maalum, wanachuoni, wanafalsafa, watu wa kalamu au wafalme ambao wana njia ya kumfikia Allaah mbali na njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili ya kutakasa fikira yao wanatumia hoja Hadiyth zilizozuliwa ambazo ni kufuru na uongo mkubwa.

Kadhalika wanatumia hoja kwa Khadhir na Muusa (´alayhimaas-Salaam) na kusema kwamba baadhi ya mawalii hawahitajii kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ambavyo Khadhir hakuhitajia kumfuata Muusa.

Mfano mwingine ni kwamba baadhi wanasema kuwa walii wa mwisho ana njia yake binafsi ya kumfikia Allaah na ndio maana hahitajii kumfuata Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano na fikira kama hizo ni nyingi kati ya wale ambao wanajinasibisha na kuipa nyongo dunia, ufukara, Taswawwuf, kalamu na falafsafa. Ukafiri wa watu hawa unaweza kuwa katika aina ya ukafiri wa mayahudi na manaswara. Unaweza ukawa mkubwa zaidi au mwepesi kidogo, kutegemea na hali zao.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (24/339)
  • Imechapishwa: 09/02/2019