Swali: Je, Suufiyyah waliokuwa baada ya Maswahabaha katika zama za Taabi´uun ´Aqiydah yao ni kama ya Suufiyyah waliokuja nyuma?

Jibu: Sikumbuki kuwa katika zama za Taabi´uun walikuwepo Suufiyyah. Suufiyyah walizuka nyuma na wanatofautiana. Kuna ambao ni Suufiyyah kwa maana ya watu wenye kuipa nyongo dunia na wenye kujitahidi katika ´ibaadah. Mfano wa hao ni Bishr bin Haafiy na Fudhwayl bin ´Iyaadhw. Hawa Suufiyyah yao ilikuwa na maana ya kuipa nyongo dunia na kujitahidi katika ´ibaadah. Lakini hata hivyo walikuwa wakifuata Sunnah ingawa walikuwa ni wenye kujiwekea uzito baadhi ya mambo. Pamoja na hivyo walikuwa wakifuata Qur-aan na Sunnah. Wale wa mwanzo wao walikuwa sawa. Lakini kila ambavyo zama zinakwenda madhehebu ya Suufiyyah yanazidi na mpaka kiasi cha kwamba yamefikia katika kufuru na ukanamungu. Kama mfano wa Ibn ´Arabiy, al-Hallaaj, Ibn Faarigh na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (04) http://alfawzan.af.org.sa/node/2047
  • Imechapishwa: 10/11/2016