Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“al-Junayd ameeleza kwamba Abu Sulaymaan ad-Daaraaniy amesema:

“Wakati mwingine ilikuwa inaweza kutokea nasikia nukta kutoka katika nukta za watu ambayo inakita kwa masiku mengi. Siikubali isipokuwa kwa mashahidi wawili waadilifu kutoka katika Qur-aan na Sunnah.”[1]

al-Junayd huyu alikuwa ni katika viongozi wa Suufiyyah. Lakini hata hivyo alikuwa katika Suufiyyah wa kati na kati. Wale Suufiyyah wa mwanzo. Walikuwa kati na kati na hawaendi kinyume na Sunnah. Walikuwa wakifanya bidii katika ´ibaadah na wakifuata Sunnah. Mmoja wao ni al-Junayd.

[1] Ighaathat-ul-Lahfaan (1/91).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (33) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%2023%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 08/02/2018