Suufiy Au Hizbiy Ndiye Asemae Maneno Kama Haya!

Swali: Baadhi ya watu wanasema:

“Nyinyi mnatazama maneno waliyosema Salaf kuhusu watu wa Bid´ah, katika Mu´tazilah, Qadariyyah na kadhalika na mnawahukumu kwayo watu.”

Jibu: Ni nani huyo ambaye tumemhukumu kwa maneno haya? Ungemtaja. Nachelea aliyesema hivi ikawa ni Suufiy, Hizbiy na mfano wao ndio huleta utata kama huu. Salaf walikuwa wakiwafanyia Tabdiy´watu wengi, muhimu ni kuangalia walikuwa katika haki au batili. Walipokuwa wakiona wamekosea walikuwa wanajirudi, na wakiona wako katika usawa ni haki. Huenda waliyemfanyia Tabdiy´ alikuwa na fikira za Rawaafidhw, Murji-ah, Khawaarij n.k. Anapokuja mtu ambaye ni Salafiy akafuata manhaj ya Salaf kwa Ahl-ul-Bid´ah, wanamtia humo kama yuko na kitu katika Bid´ah hizi. Watu wengi wanataka kuishi kwa fikira za Ahl-ul-Bid´ah kisha hawataki waongelewe watu wa Bid´ah. Wanawapenda watu wa Bid´ah, wanawatetea mpaka kwa fikira potofu waliyomo, hata imekuwa [unapojitokeza kutaka] kuitetea haki wanakupiga vita na wewe. Utakuta kuna mtu anawatukana Mitume na Maswahabah, wamtetea mtu huyu na Bid´ah hizi. Yapi maoni yako kwa mtu ambaye anamtetea yule ambaye kamtukana Mtume Muusa, Maswahabah na ana imani ya Huluul ilihali mtu huyo anajinasibisha na Salafiy? Unamtia katika Bid´ah. Aina ya watu kama hawa ni shari kuliko hata Ahl-ul-Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=355
  • Imechapishwa: 09/11/2014