Sutrah kwa anayeswali msikiti Makkah Mtakatifu wa Makkah

Swali: Ikiwa mtu anaswali Rak´ah mbili katika msikiti Mtakatifu wa Makkah ni lazima kwake aweke Sutrah?

Jibu: Hapana, si lazima akiwa katikati ya msikiti Mtakatifu kutokana na msongamano mkubwa. Ipo Hadiyth dhaifu kuhusu kutokuweka Sutrah. Hata hivyo kinachozingatiwa ni ule msongamano na ugumu katika Sutrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21627/حكم-اتخاذ-السترة-للمصلي-في-الحرم-المكي
  • Imechapishwa: 30/08/2022