Suruuriyyuun ni watu gani?


Suruuriyyah ni unasibisho kwa Muhammad Suruur Zayn-ul-´Aabidiyn, mtu mwenye [kitabu kiitacho] “Manhj al-Anbiyaa´.” Kitabu cha udanganyifu kwa kichwa cha khabari yake, kinachoharibu tabia,´Aqiydah na kinalingania katika ´Aqiydah ya Khawaarij, kinachowaharibu vijana, kinachotoa malezi juu ya uhayawani na kutokuwa na hayaa, matusi, kulaani na Takfiyr. Hii ndo Suruuriyyah. Je, Muhammad Suruur na wafuasi wake wameshawahi siku yoyote kuwaandikia viongozi hawa [na kuwanasihi]? Ni kweli ya kwamba wengi wao ni matwaghuti kwa kuwa wanahukumu kinyume na aliyoteremshaAllaah. Lakini je, njia ya kutengeneza ni kutukana na Takfiyr? Au njia ya kutengeneza ni Ahl al-Hall wa al-´Aqd katika wanachuoni na wenye busara wakutane na kuwaandikia viongozi hawa.

“Enyi viongozi kumbukeni nyinyi ni waislamu na mnaowaongoza ni waislamu na mnahukumu nchi ya Kiislamu. Ni juu yenu kirejea katika Kitabu cha Allaah na muwaongoze watu kwa Shari´ah ya Allaah.”

Na je, [Muhammad] Suruur na watu mfano wake wameshawahi kufanya kitu kama hichi? Kisha unaposema ya kwamba viongozi wote ni matwaghuti, hujasoma “Baab-ul-Istithnaa´”? Huna kubagua wewe? Je, leo duniani hakuna viongozi ambao sio matwaghuti? Mtu huyu aliishi katika nchi hiikipindi fulani na anajua ´Aqiydah ya nchi hii, hukumu ya nchi hii na hukumu za nchi hii. Anajua haya vizuri. Lakini kutokana na ujinga hajui na ndio maana akakufurisha wote, akawahukumu [viongozi] wote kuwa ni matwaghuti na vijana wakamfuata kichwa mchunga. Hii ndio Suruuriyyah kwa kifupi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.eljame.com/mktba/catplay.php?catsmktba=3
  • Imechapishwa: 05/09/2020