Sunnah ya Raatibah inamtosha mtu kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid

Swali: Je, Sunnah ya Raatibah inamtosheleza mtu kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid?

Jibu: Sunan za Rawaatib zilizohifadhiwa katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Rak´ah kumi na mbili; Rak´ah nne kabla ya Dhuhr kwa salamu mbili, Rak´ah mbili  baada ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Maghrib, Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa na Rak´ah kabla ya Fajr. Hizi ndio Sunan za Rawaatib. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kuzihifadhi.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Allaah amrehemu yule mtu ambaye ameswali [Rak´ah] nne kabla ya ´Aswr.”

 Imependekezwa kuziswali kabla ya ´Aswr. Lakini haziingii ndani ya Raatibah.

Pia mtu anaweza kuswali baina ya adhaana na Iqaamah; Rak´ah mbili baada ya adhana ya Maghrib na baada ya adhaana ya ´Ishaa. Mtu afanye hivo katikati ya adhaana na Iqaamah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah. Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah.”

Bi maana adhaana na Iqaamah. Hizi zimependekezwa na sio Raatibah. Mtu aswali Rak´ah mbili baada ya adhaana ya Maghrib na baada ya adhaana ya ´Ishaa. Lakini mtu akiswali Tahiyyat-ul-Masjid atakuwa amefikia malengo. Mtu akiswali Rak´ah mbili wakati wa kuingia msikitini atakuwa amefikia malengo.

Kadhalika Sunan za Rawaatib mtu akiziswali msikitini atakuwa amefikia malengo. Mambo ni namna hii mtu akiswali Sunnah ya Fajr msikitini atakuwa amefikia malengo na zinamtosha kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7045/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D8%AD%D8%AF%D9%89-%D8%A7%D8%B0%D9%86%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D9%84%D9%88%D8%AF-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%82%D8%A7%D9%85%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AE%D8%B1%D9%89
  • Imechapishwa: 13/06/2019