Sunnah usiku wa kuamkia ´Iyd


Swali: Je, kuna Sunnah maalum inayofanywa usiku wa kuamkia ´Iyd?

Jibu: Sijui Sunnah yoyote maalum ya kufanywa usiku wa kuamkia ´Iyd zaidi ya kile kinachotambulika na Takbiyr iliyothibiti katika maneno Yake (Ta´ala):

وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

“Ili mkamilishe idadi na ili mumkabiri Allaah kwa kuwa amekuongozeni na ili mpate kushukuru.”[1]

Kumepokelewa Hadiyth kuhusu fadhilah za kuhuisha usiku wa kuamkia ´Iyd, lakini wanachuoni wameitia dosari na ndio maana sithubutu kuzungumzia kitu chochote maalum.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/209-210)
  • Imechapishwa: 14/06/2018