Sunnah ni kusoma du´aa kimyakimya

Swali: Baadhi ya watu wanasoma du´aa kwa sauti ya juu ambapo wanawashawishi walioko pambizoni mwao. Ni ipi hukumu ya kitendo chao?

Jibu: Sunnah ni kusoma du´aa kwa sauti ya kimyakimya ndani ya swalah na nje ya swalah. Allaah (Subhaanah) amesema:

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye hawapendi wenye kuvuka mipaka.”[1]

Jengine pia ni kwa sababu kufanya hivo ndio kamilifu zaidi katika Ikhlaasw na moyo unakusanyika juu ya du´aa. Isitoshe kufanya hivo hakuwashawishi wale waswaliji na wasomaji Qur-aan walioko kando naye. Isipokuwa pale ambapo du´aa ni miongoni mwa zile zenye kuitikiwa “Aamiyn”. Katika hali hiyo imamu atatakiwa kusoma kwa sauti ya juu ili wasikilizaji waitikie “Aamiyn”.

[1] 07:55

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/125)
  • Imechapishwa: 22/10/2021