Sunnah katika swalah ya ´Iyd ni jangwani na sehemu palipo wazi na si msikitini

Swali: Ni ipi Sunnah katika swalah ya ´Iyd? Je, watu waswali msikitini au jangwani? Ikiwa jibu ni kwamba watu waswali jangwani mji unaendelea kupanuka na kila ambapo kunatengwa mahali pa kuswalia kwa ajili ya ´Iyd basi majengo yanajengwa pembezoni mwake na kunakuwa hakuna ule wasifu wa kwamba ni jangwani.

Jibu: Sunnah katika swalah ya ´Iyd iswaliwe jangwani. Hivo ndivo alivokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mji ukipanuka basi inatakiwa kuhamisha sehemu ya kuswalia kwenda jangwani. Ikiwa hilo haliwezekani basi hakuna neno. Kwa sababu uwanja wa kuswalia kuwa jangwani sio kwa njia ya uwajibu. Bali ni kwa njia ya mapendekezo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/233)
  • Imechapishwa: 14/06/2018