Subira ya al-Bukhaariy juu ya matusi na dhuluma

 Muhammad bin Abiy Haatim amesema:

“Bwana mmoja alikuja kwa Abu ´Abdillaah na akasema: “Ee Abu ´Abdillaah! Kuna mtu anasema kuwa wewe ni kafiri.” Akasema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu akimwambia nduguye “Ee kafiri!”, basi ni lazima impate mmoja wao.”[1]

Marafiki zake wengi walikuwa wakimwambia kwamba baadhi ya watu wanamtukana, lakini anasoma tu:

إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا

”Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.” (04:76)

وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ

”Lakini vitimbi viovu havimzunguki isipokuwa mwenyewe.” (35:43)

´Abdul-Majiyd bin Ibraahiym alimwambia: “Kwa nini humuombi Allaah dhidi ya wale wanaokudhulumu, wanaokutukana na kukusemea uongo?” Akajibu: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Subirini mpaka mtapokutana nami kwenye Hodhi.”[2]

“Yule mwenye kuomba dhidi ya mkandamizaji wake basi ameshinda.”[3]

[1] Maalik (3/148), Ahmad (2/113), al-Bukhaariy (10/428), Muslim (60) na at-Tirmidhiy (2637).

[2] al-Bukhaariy (7057) na Muslim (1845).

[3] at-Tirmidhiy (3552). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (3552).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/418-419)
  • Imechapishwa: 06/12/2020