Soksi zinapanguswa vipi?


Swali: Ni vipi mtu anapangusa juu ya soksi? Ni yepi masharti yake?

Jibu: Inafaa kupangusa soksi ikiwa zinafunika nyayo na vifundo vya miguu. Ni kama ambavo inafaa kupangusa juu ya soksi za ngozi ikiwa mtu amevaa soksi za kawaida na soksi za ngozi hali ya kuwa na twahara kamili. Mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mkazi na michana mitatu na nyusiku zake kwa msafiri. Muda unaanza kuhesabiwa kuanzia mpanguso wa kwanza baada ya kupatwa na hadathi. Kwa sababu imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh yanayofahamisha juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/106)
  • Imechapishwa: 14/08/2021