Siwaak wakati wa darsa na wakati wa kumuitikia muadhini

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak wakati wa darsa na wakati wa kumuitikia muadhini?

Jibu: Hakua neno wala ubaya. Kilichokatazwa ni kutumia Siwaak ndani ya swalah na wakati wa kusikiliza Khutbah. Ni lazima kusikiliza Khutbah ya ijumaa na wala haifai kwa mtu kuzungumza ndani yake kama ambavo haifai kwake akazungumza wakati wa swalah, asimuitikie anayemtolea salamu kwa mkono wake na wala asimjibu anayechemua. Ama ndani ya darsa na wakati wa kumuitikia muadhini ni jambo halina neno.

Mtu akiuliza kama inafaa kuitikia “Aamiyn” na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa Khutbah? Ndio, hakuna neno. Ayafanye hayo baina yake yeye na nafsi yake ambapo aitikie “Aamiyn” na amswalie  Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu mambo haya sio katika mazungumzo ya watu. Kilichokatazwa ni mazugumzo ya watu. Vivyo hivyo asiguse vijiwe, asicheze katikati ya Khutbah, asitumie Siwaak, asimtakie rehema mwenye kuchemua na wala asiitikie salamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 23/02/2020