Swali: Je, ni Sunnah kusafisha meno kwa Siwaak baina ya Khutbah mbili za ijumaa? Naona maimamu wengi wanafanya hivo.

Jibu: Haina neno. Kilichokatazwa ni kutikisika na matendo wakati wa Khutbah. Kuhusu baada ya Khutbah au baina ya Khutbah mbili haina neno. Kwa mfano haina neno kumwambia aliye pambizoni mwako kuchukua kitu au kupeana kitu baina ya Khutbah mbili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 09/10/2016