al-Halabiy amesema:

“Sisi tunapomtoa mtu nje ya Salafiyyah haitakikani iwe ni jambo la kufuata kichwa mchunga. Inatakikana iwe ni jambo lililojengwa juu ya elimu, dini na dalili. Pale ambapo dalili itatudhihirikia basi – Allaah akitaka – hatutokuwa na kiburi na kuzidhulumu nafsi zetu kwa kupingana na haki na kwenda kinyume na wanachuoni.”

Allaah anajua kuwa sisi hatumfuati kichwa mchunga yeyote wala kutenda kiurafiki na yeyote. Tunatendea kazi dalili iliyosihi kwetu. Sisi sio katika wale ambao wanamfuata mtu kichwa mchunga katika mambo haya au kutenda kiurafiki kwa mwengine pasi na haja. Wala hatumtuhumu yeyote kwa hilo. Ikiwa mpaka sasa bado hujabainikiwa kuwa al-Maghraawiy ni Khaarijiy basi na usome kipeperushi kilichokusanywa na Salafiyyuun Marocco.

Sisi hatuhitajii kwa yeyote kufuata kitu ambacho ni kosa, lakini tunachohitajia ni kwamba wanachuoni wenye kujinasibisha na Salafiyyah wawe na umoja katika kuinusuru haki na kuitupilia mbali batili kwa ajili ya Allaah Pekee.

Lengo sio sisi kuwa wengi. Tunaomba kinga kwa Allaah kutokana na hilo. Sisi tunaamini kuwa haki ni yenye kunusuriwa hata kama mwenye kushikamana nayo atakuwa ni mtu mmoja tu na tunaamini vilevile kuwa batili ni yenye kuangushwa hata kama watu wote wataiangukia. Tuna mafunzo kwa Mitume wa Allaah. Allaah alimnusuru Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya nguvu zote za ulimwengu kukusanyika dhidi yake na kuuambia moto ambao walikuwa wamekonga kwa ajili ya kumtupa ndani yake:

كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ

“Kuwa baridi na salama juu ya Ibraahiym.“ (21:69)

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 380-381
  • Imechapishwa: 18/03/2017