Sisi tunahukumu kwa mujibu wa uinje na ya ndani yanajua Allaah pekee

Swali: Tunasoma kwako vichenguzi vya Uislamu na siku zote unaashiria kwamba ambaye anafanya kadhaa basi ni kafiri. Hapana shaka kwamba unakusudia kwa njia ya ujumla. Kwa ajili ya kuondosha utata wako ambao wanazipachika hukumu hizi kwa mtu mmoja mmoja pasi na kuhakikisha masharti wala kutokuwepo vikwazo. Tunaomba ubainifu na kuwekewa wazi jambo hili?

Jibu: Ndio, kumkufurisha mtu kwa dhati yake ikiwa mtu huyo hana udhuru hapana shaka kwamba anakufurishwa. Anayemsujudia asiyekuwa Allaah anakufuru. Anayemchinjia mwingine asiyekuwa Allaah anakufuru. Sisi tunampa hukumu ya ukafiri. Isipokuwa akitubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na akajirudi. Basi itambulike kuwa mwenye kutubia Allaah anamsamehe. Sisi tuna jengine cha kuangalia isipokuwa ule uinje. Hatuna uwezo wa kupekua yaliyomo moyoni. Hayo tunamwachia Allaah. Mwenye kufanya matendo, ya kimaneno au kivitendo, tunamhukumu ukafiri. Mwenye kufanya shirki au akatamka shirki, tunamhukumu ukafiri. Sisi hatuna cha kuangalia isipokuwa ule uinje. Hukumu zinaangalia ule uinje. Kuhusu  yaliyomo ndani ya moyo Allaah pekee ndiye mwenye kuyajua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (06)
  • Imechapishwa: 25/12/2018