Siri iliyopo ya kuitikiwa du´aa

Ni jambo lenye kujulikana ya kwamba kuitikiwa Du´aa ni katika athari ya uola wa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa viumbe Wake. Kutokana na hili, kuitikiwa Du´aa haiwi kwa muumini peke yake pasina kafiri. Bali kafiri na muovu wanaweza kuitikiwa pia. Bali hata Ibliys aliitikiwa. Kwa kuwa kuitikiwa Du´aa ni miongoni mwa athari za uola, kama mfano wa riziki ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa viumbe Wake na kuwapa vitu vingine wanavyoweza kuwa wanahitajia. Hivyo basi, mnaswara anaweza kuomba na akaitikiwa Du´aa yake. Vilevile mshirikina na kadhalika.

Kuitikia huku sio kwa sababu anakustahiki, isipokuwa ni kwa sababu ndani ya moyo wake kumepatikana unyenyekevu, dhiki na haja kwa Mola Wake (Jalla wa ´Alaa). Uola ni kwa muumini na kwa kafiri pia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 196
  • Imechapishwa: 16/05/2020