Sio Sunnah kupangusa shingo wakati wa kutawadha

Swali: Kufuta shingo wakati wa kutawadha sio jambo lililopendekezwa? Kwa sababu ni jambo linalofanana na mayahudi kama nilivyosikia.

Jibu: Ndio, haikupendekezwa. Wala haikuwekwa katika Shari´ah kupangusa shingo. Kinachopanguswa ni kichwa na masikio mawili peke yake. Hivo ndivo imefahamisha Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/102)
  • Imechapishwa: 13/08/2021