Swali: Ni ipi njia sahihi ya kusoma Fiqh kwa mwanafunzi? Je, afuate madhehebu maalum au asome somo la Fiqh moja kwa moja? Wanachuoni wengi wa zama hizi wanamshauri mwanafunzi afuate madhehebu maalum halafu kupitia madhehebu hayo atajiendeleza kusoma Fiqh.

Jibu: Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

”Walisema: “Hatoingia Peponi isipokuwa aliyekuwa myahudi au mnaswara.” Hilo ni tamanio lao. Sema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli”.” (02:111)

Leteni dalili juu ya kwamba ni wajibu kwa mtu kufuata madhehebu maalum. Sio wajibu kumfuata yeyote katika madhehebu yake na mfumo wake isipokuwa tu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ninakhofia akijiingiza kwenye madhehebu maalum hatoweza kutoka humo na akawa ni mtu mwenye kasumba na kupuuza Sunnah na watu wa Sunnah. Hili ni nadra sana kutokea.

Ninamnasihi asome na kuhifadhi Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kiasi na atakavyoweza. Vilevile asome vitabu vya Fiqh-us-Sunnah ambavyo vitamnufaisha kwa kuvisoma kuweza kuitambua Fiqh sahihi na ilio safi. Aisome moja kwa moja kwa dalili zake kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Vilevile itamnufaisha kuweza kutambua lugha ya Qur-aan na Sunnah. Vilevile itamnufaisha kuweza kutendea kazi kanuni za misingi ya Fiqh. Vilevile itamnufaisha kuweza kutendea kazi kanuni za misingi ya Hadiyth.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12067
  • Imechapishwa: 06/09/2020