“Simtaki tena mke wangu” – je, ni talaka?

Swali: Kumetokea mgogoro kati yangu mimi na familia ya mke wangu wakati ambapo mke wangu alizaa hospitalini na baba yake akanitaka nimpeleke kwa familia ya mke wangu lakini hata hivyo nikakataa. Baada ya hapo nikampeleka nyumbani kwa familia yake na akabaki huko kwao. Wakati nilipotaka kumchukua wakakataa. Baadaye mamangu akaniuliza ni wapi yuko mke wangu ambapo nikamjibu kuwa simtaki tena. Je, maneno yangu “simtaki tena” yanahesabiwa ni talaka?

Jibu: Hapana, sio talaka. Isipokuwa ikiwa ulikusudia kwayo talaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3556/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%B9%D8%AF-%D8%B7%D9%84%D8%A7%D9%82%D8%A7-%D9%85%D9%86-%D9%82%D8%A7%D9%84-%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%AA%D9%87-%D9%84%D8%A7-%D8%A7%D8%B1%D8%BA%D8%A8%D9%83
  • Imechapishwa: 29/02/2020