´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu kunyanyua sauti yake pindi anaposoma Qur-aan kabla na baada ya ´Ishaa ambapo akawashawishi marafiki zake wanaoswali.”

Hadiyth hii cheni ya wapokezi ni njema.

Ndani ya Hadiyth yapo makatazo ya usomaji wa Saba unaofanyika katika baadhi ya misikiti pindi watu wanaswali. Kitendo kama hicho kinawashawishi waswaliji. Hapo ni pale ambao watasoma kisomo kinachofaa na cha utaratibu. Lakini ikiwa kisomo ni cha harakaharaka na kumeza maneno, basi ni haramu. Naapa kwa Allaah kwamba limeeneza uharibifu, Bid´ah kushinda na kufichikana kwa Sunnah. Wamekuwa wachache wenye kusimama kwa haki. Bali endapo mwanachuoni atatamka kwa ukweli na ikhlaasw, basi atapingwa na idadi kadhaa ya wanachuoni wa wakati wake, kuchukiwa na kumfanyia ujinga.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/165-166)
  • Imechapishwa: 11/11/2020