Silimu kwanza kisha ndio uoge


141- Nilimuuliza baba yangu kama msalimu analazimika kuoga. Akajibu:

“Imesemekana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwamrisha msilimu kuoga; Hadiyth ya Qays bin ´Aaswim.”

Nilimuuliza baba yangu:

“Na ikiwa alioga kabla ya kusilimu?”

Akajibu:

“Hapana. Msilimu anatakiwa kuoga kwa sababu ya kule kuacha ukafiri wake. Hata hivyo hawa wanasema kuwa ni sawa kuoga kwanza kisha ndio mtu asilimu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/113)
  • Imechapishwa: 06/02/2021