Sikukuu za makafiri kama krismasi na za waislamu kama maulidi

Swali: Ipi hukumu ya kusherehekea sikukuu, iitwayo “Sikukuu ya manaswara”, au “Krismasi”. Ipi nasaza yako kwa waislamu ambao wanashiriki katika hili na wanapeana zawadi na kuwapa pongezi n.k.?

Jibu: Haijuzu kwa Muislamu kushiriki sikukuu za manaswara – hata sikukuu za waislamu ambazo zimezushwa. Kama maulidi na kadhalika, sherehe ya maulidi – haijuzu kwa kuwa ni sherehe za Bid´ah.

Na sikukuu za manaswara ni sikukuu za Bid´ah na shirki, kwa kuwa wao hufanya kwa kuitakidi kama ´ibaadah kwa ´Iysaa (´alayhis-Salaam).

Haijuzu kuwashaji´isha kwa hili wala kuwapongeza. Kule kuwapa tu pongezi ni jambo lisilojuzu. Vipi kwa yule ambaye anahudhuria kwao? Hata kuwauzia, asiwauzie mtu vifaa ambavyo vitawasaidia kufanya hayo maulidi. Wala mtu asiwape pongezi kwayo, wala asiwauzie kwa haya maulidi na wala asile katika kichinjo chao. Muislamu anatakiwa awasuse kabisa kwa haya maulidi.

Kama alivyosema hilo al-´Allaamah Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn-ul-Qayyim katika kitabu “Ahkaam Ahl-idh-Dhimmah.”

Ni wajibu kujiweka mbali kuwashiriki katika mambo haya, kwa kuwa haya ni katika Dini yao. Na sisi tumekatazwa kuwashaji´isha au kuwasaidia katika kufuru zao na shirki zao.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/-wHD0HfeV18
  • Imechapishwa: 06/10/2020