Siku za kufanya ´Aqiyqah


Swali: Inafaa kumchinjia mtoto kichinjwa katika siku mbali na tarehe saba, tarehe kumi na nne au ishirini na moja? Imeshurutishwa iwe katika masiku yasiyogawanyika? Ni lipi bora kuchinja na kuigawanya au kutengeneza chakula na kualika watu?

Jibu: Sunnah ni kufanya ´Aqiyqah katika ile siku ya saba[1] kutokana na yaliyothibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila mtoto ni mwenye kuwekewa rehani kwa ´Aqiyqah yake. Anachinjiwa ile siku ya saba.”

Wanachuoni wamesema endapo mtu atapitwa na hiyo siku ya saba, basi afanye tarehe kumi na nne. Ikimpita hiyo siku tarehe kumi na nne, basi afanye tarehe ishirini na moja. Akipitwa na siku hizo basi afanye siku yoyote. Ni mamoja yawe masiku ya kugawanyika au masiku yasiyogawanyika. Lakini hata hivyo Sunnah ni yeye kufanya tarehe saba. Hili ndio bora zaidi. Ikishindikana basi afanye siku yoyote. Mtoto wa kiume anachinjiwa mbuzi/kondoo wawili. Mtoto wa kike anachinjiwa mbuzi/kondoo mmoja.

Mtu anatakiwa kutazama kile ambacho ni bora na chenye manufaa zaidi. Endapo ataigawanya kwa majirani na kwa ndugu kuna mtazamo wa kufanya hivo. Iwapo vilevile atawakusanya majirani na marafiki ni sawa. Ni mwenye khiyari ya kufanya kati ya hayo mawili.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/aqiyqah-siku-ya-nane/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 23/03/2018