Siku ya wapendanao ni sikukuu ya kinaswara

Swali: Kumekuja maswali mengi juu ya siku ya wapendanao (Valentine). Wanataraji kama unaweza kubainisha khatari ya kusherehekea sikukuu hii na kamati ya al-Lajnah ad-Daaimah itoe fatwa kuhusu hilo.
Jibu: Siku ya wapendanao? Ni sikukuu ya kinaswara. Haijuzu kwa Waislamu kushiriki katika hilo. Haitakiwi kwao kuita katika hilo kama jinsi haitakiwi vilevile kushuhudia uongo. Hii ni sikukuu ya makafiri na haitakiwi kuita katika hilo.

Mapenzi haya ni kwa nani? Kwa Iblisi? Au kwa al-Masiyh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Au ni mapenzi kati yao? Hakuna mapenzi kati yao ikiwa ni makafiri:

تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ

“Utawadhania wako pamoja, kumbe nyoyo zao ziko mbalimbali.” (49:14)

Wanasema kwamba ni mapenzi kwa nisba ya mwanamke? Ni uasherati.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/alla-hjartans-dag-ar-en-kristen-hogtid/
  • Imechapishwa: 14/02/2017