Siku tatu mfululizo badala ya siku thelathini

Swali: Je, mtu anaweza kufunga siku tatu mfululizo usiku na mchana katika Ramadhaan na ikawa ni badala ya siku thelathini?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo na wala hayajasemwa na mwanachuoni yeyote. Usiku sio sehemu ya kufunga. Yeyote atakayefanya hivo anazingatiwa ameenda kinyume na Shari´ah takasifu na amefanya mambo ambayo hayakuwekwa na Allaah katika Shari´ah na amekula ndani ya Ramadhaan pasi na udhuru. Jengine ni kwamba Allaah (Subhaanah) amewajibisha kwa watu na majini ambao ni waislamu kufunga Ramadhaan yote. Kwa hivyo haisihi kufunga baadhi ya siku kutokamana na nyenginezo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/88) nr. (3089)
  • Imechapishwa: 24/04/2022