Sijda ya kusahau akiacha du´aa ya Witr au ameacha kusoma kwa sauti ya juu?

Swali: Ninaposahau du´aa ya Witr nalazimika kusujudu sijda ya kusahau? Vilevile wakati sisomi kwa sauti ya juu katika wakati ambao ni lazima kusoma kwa sauti ya juu na nimefanya hivo kwa kusahau?

Jibu: Si lazima mtu akiacha Qunuut kwa kusahau au asisomi kwa sauti ya juu katika swalah ya kusoma kwa sauti ya juu kwa kusahau. Haimlazimu kusujusu sijda ya kusahau. Lakini hapana neno akisujudu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/278)
  • Imechapishwa: 02/11/2021