Sifa za mnyama wa ´Aqiyqah na Udhhiyah


Swali: Ni sifa zipi mnyama anatakiwa kuwa nazo mnyama anayechinjwa katika ´Aqiyqah? Je, inatakiwa kugawanywa mara tatu kama mnyama wa Udhhiyah?

Jibu: Hukumu za Udhhiyah ni kama za ´Aqiyqah kikamilifu. Kondoo anatakiwa kuwa ametimiza miezi sita, mbuzi anatakiwa kuwa ametimiza mwaka mmoja, ng´ombe anatakiwa kuwa ametimiza miaka miwili na ngamia anatakiwa kuwa ametimiza miaka tano. Mnyama anatakiwa kuwa amesalimika na kasoro kama kuwa kipofu, mwenye kusunda, mgonjwa au mzee.

Kuhusu nyama yake, Sunnah anatakiwa kugawanywa sehemu tatu; sehemu ya kwanza ni ya kwake yeye na familia yake, sehemu nyingine aitoe swadaqah na nyingine awape watu wa karibu yake na wapenzi wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/05/2018