´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kila kitu ni kwa Qadar, mpaka kushindwa na werevu.”[1]

Qadar hii imekusanya hali zote za mja, matendo yake na sifa zake, mpaka kushindwa na werevu. Hizi ni sifa mbili zilizo kinyume. Sifa ya kwanza, ambayo ni kushindwa, inapelekea katika kutokuweza na ukhasirikaji. Sifa ya pili, ambayo ni werevu, ambao unapelekea kuwa na bidii katika kumtii Allaah.

Ushindwaji unaokusudiwa hapa ni ule wenye kusemwa vibaya ambao una maana yake ni kule mtu kutokuwa na matakwa. Kwa msemo mwingine uzembe. Haihusiani na ushindwaji wa kutokuwa na uwezo. Hii ndio maana ya Hadiyth ya ile Hadiyth nyingine inayosema:

“Tendeni! Kila mmoja amewepesishiwa kwa lile aliloumbiwa. Kuhusu wale wenye furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yenye furaha na wale wasiokuwa na furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yasiyokuwa na furaha.”[2]

Kuhusu wale wenye furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yenye kuwafanya wakawa na furaha. Hayo ni kutokana na werevu wao, mafanikio yao na upole wa Allaah juu yao.

[1] Muslim (2655), Ahmad (5859) na Maalik (1663).

[2] al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjatu Qulûb-il-Abraar, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 21/02/2019