Swali: Ni zipi sifa za kipekee za mwezi wa Muharram? Je, madhambi ndani yake yanaongezwa?

Jibu: Miongoni mwa sifa maalum za mwezi wa Muharram ni kwamba ni mwezi mtukufu na kufanya dhambi ndani yake ni khatari. Amesema (Ta´ala):

فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ

“Hivyo basi msijidhulumu humo nafsi zenu.”[1]

Vivyo hivyo matendo mema yanaongezwa na khaswa ukizingatia ya kwamba mwezi wa Muharram kuna swawm ilio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swawm bora baada ya mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Allaah ambao mnauita “Muharram.”

[1] 09:36

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 06/12/2018