Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

22- Abu ‘Abdillaah Jaabir bin ‘Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kuna mtu alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unafikiriaje lau nitaswali swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nihalalishe halali na nikaharimisha haramu na nisifanye jambo lolote jengine nitaingia peponi? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu: “Ndio.”

Imepokelewa na Muslim.

Hadiyth hii inaonyesha dalili ya kwamba mwenye kuyafanya mambo haya ya wajibu hali ya kuwa ni mwenye kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall), akaswali swalah za faradhi kwa kumtii Allaah (´Azza wa Jall), akafunga na kutoa zakaah kwa kumtii Allaah, akahiji kwa kumtii Allaah, akahalalisha halali na kuharamisha haramu kwa kumtii Allaah, mtu huyu ni katika watu wa Peponi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 310
  • Imechapishwa: 14/05/2020