Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

15- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze [mambo ya] kheri au anyamaze; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu jirani yake; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake.”

Hadiyth hii inafahamisha kuwa miongoni mwa sifa za mwenye kumuamini Allaah na siku ya Mwisho, ambaye anamuogopa na kumcha Allaah, anaogopa yatayompitikia Aakhirah na anataraji kuwa ni mwenye kuokoka Aakhirah, miongoni mwa sifa zake ni kuwa:

1- Anazungumza mambo ya kheri au hunyamaza.

2- Anamkrimu jirani yake.

3- Anamkirimu mgeni.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 237
  • Imechapishwa: 14/05/2020