al-Hajuuriy amesoma na kutoa idhini kutoka kitabu – kama ilivyo katika anwani – ambapo mwandishi wa kitabu hicho anasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakubaliwi maneno yake isipokuwa kwa dalili au hoja yenye kukubaliwa.

Tazama namna ulivyo ujinga wa mwandishi! Hivi huyu mwandishi na mpitiaji – yaani al-Hajuuriy – hawajui kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazungumzi isipokuwa haki na wala hasemi isipokuwa ukweli? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hasemi na wala hafanyi katika yale yanayohusiana na dini isipokuwa kwa Wahy kutoka kwa Allaah (Ta´ala).

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/11)
  • Imechapishwa: 11/10/2016