Inatakikana kwa mtu asiyekuwa asiyejishughulisha na mambo ya elimu kutomuuliza Muftiy dalili. Wala haifai kwake kusema: “Kwa nini umesema.. ?”

Kama atapenda kuituliza nafsi yake kwa kusikiliza dalili, basi aitafute [kutoka kwa mwanachuoni huyo] katika kikao kingine au katika kikao hichohicho lakini baada ya kuwa ameshakubali hiyo fatwah kavu.

Si vibaya Muftiy wakati wa kutoa fatwa yake kutaja dalili ikiwa ni andiko lililo wazi na fupi.

asw-Swaymariy amesema:

“Asitaje dalili pindi anapomjibu mtu asiyejishughulisha na mambo ya elimu na aitaje wakati anapomjibu mtu ambaye ni msomi. Kama mfano wa mtu anayemuuliza mwanamke kuolewa bila walii ni vyema akanukuu kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna ndoa bila ya walii.”

Au kumrejea mwanamke ambaye mtu amemwacha baada ya kumwingilia ambapo akanukuu kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:

وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ

“Waume zao wana haki kuwarejea.” (02:228)

  • Mhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/52)
  • Imechapishwa: 29/12/2019