Si lazima kutanguliza nia ya uimamu ili uwaswalishe watu

Swali: Niliingia kuswali Dhuhr baada ya takriban saa moja na swalah ya mkusanyiko ilikuwa imemalizika na wakati nilipokuwa katika katika Rak´ah ya kwanza waliingia watu wawili wakajiunga nami. Lakini sikuwa nimenuia swalah ya mkusanyiko katika hali hii. Je, swalah zao zinasihi?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba haikushurutishwa kwa imamu kuweka nia ili awe imamu. Bali inasihi kwake kuwaongoza watu ijapo hakunuia uimamu, kama sura iliyotajwa katika swali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kuswali swalah ya usiku. Baada ya kuanza swalah yake Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) akasimama upande wa kushotoni mwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamshika masikio yake na akamweka upande wa kuliani mwake[1].

Udhahiri wa Hadiyth hii ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunuia kumswalisha Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na hakujiunga naye isipokuwa baada ya kuanza swalah yake. Kwa msemo mwingine ni kwamba hakujua kuwa ataswali pamoja naye.

Kujengea juu ya haya swalah yenu nyote ni sahihi. Lakini nakunasihi kupupia kudhibiti swalah ya mkusanyiko msikitini na kutahadhari kuchelewa. Kwa sababu ni lazima kuswali na mkusanyiko msikitini. Hivyo pupia jambo hilo.

[1] al-Bukhaariy (117), Muslim (763), an-Nasaa´iy (806) na wengineo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/ar/content/نية-الإمام-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 20/06/2022