Swali: Inajuzu kwa mtu kuwalingania watu katika kijiji chake katika Da´wah Salafiyyah na wakati huohuo akawa haonyeshi kuwa ni katika watu wa Da´wah hii mpaka pale baadhi watapokubali? Bali yeye anawalingania tu katika haki.

Jibu: Mlinganizi hajitangazi kuwa yeye ni Salafiy. Anachotakiwa ni yeye kuwaambia kuwa hiki ni Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na awalinganie katika hayo. Sio lazima awatangazie kuwa yeye ni Salafiy. Awaambie hiki ni Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na awafundishe. Endapo watasema kuwa hawataki Salafiyyah. Katika hali hiyo tunamwambia kuwa itakuwa ni lazima sasa kutangaza.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda: Jalsah istiraahah as-Swafaa http://rabee.net/ar/questions.php?cat=27&id=199#
  • Imechapishwa: 11/02/2018