Si lazima kutaja mazuri ya unayemtahadharisha


Swali: Wakati tunapokataza makosa na Bid´ah ambazo wanatumbukia ndani yake watu walio na athari kwa watu na zimeenea Bid´ah zake na khaswa zinazohusiana na ´Aqiydah na kukachupwa mpaka kwazo. Wakati tunapokemea Bid´ah basi baadhi ya wanajitokeza kwa madai kwamba haki inahitaji kutaja mazuri na kasoro vyote viwili na kwamba jitihada zake katika kulingania na kutangulia kwake kunazuia kutokosolewa hadharani. Tunaomba utubianishie mfumo wa haki; je, ni lazima kutaja yale mazuri? Je, kutangulia katika ulinganizi kunazuia kutaja makosa yake yaliyoenea kati ya watu?

Jibu: Ni lazima kwa wanazuoni kukemea Bid´ah na maasi ya waziwazi kwa dalili za kidini, kupendekeza, kuogopesha na kwa njia zilizo nzuri. Sio lazima wakati wa kufanya hivo kutaja mazuri ya mzushi. Lakini yule anayefanya hivo wakati atayataja [mazuri] ya ambaye ametumbukia ndani ya Bid´ah au maovu mengine hali ya kuwa ni mwenye kumkumbusha juu ya matendo yake mazuri na kumvutia kutubu kwa Allaah basi jambo hilo ni zuri. Aidha ni miongoni mwa sababu za kukubali ulinganizi na kurejea katika kutubia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/352)
  • Imechapishwa: 24/07/2021