Si kila mmoja inafaa kumuua mchawi


Swali: Je, mchawi anauwa kwa hali zake zote hata kama ni mchawi anayeanza? Nifanye nini nikijua kuwa mchawi ni mmoja katika ndugu zangu?

Jibu: Hakuna anayemuua mchawi isipokuwa tu watawala. Sio kila mmoja anayewaua. Ni mambo maalum yanayofanywa na mtawala. Si kila mmoja inafaa kwake kutuhumu na kuua. Haijuzu. Ni vurugu. Hili halitokomezi uchawi. Mtawala ndiye anawateua watu na kuwafanyia hesabu. Ama wewe ukiingilia mambo yao ima wakuue au wawaue watoto wako. Haijuzu. Ni vurugu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (61) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid-%2029%20-0%206-1438.mp3
  • Imechapishwa: 06/08/2017