Si ISIS Wala Raafidhwhah


Swali: Kuna lolote la kusema kuhusiana na ukhalifah wa Kiislamu uliotangazwa jana?
Jibu:

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu.” (30:41)

Ufisadi unapitika ima kwa kupetuka mipaka au kwa kuchuja. Kuchuja inakuwa kwa kupitia wakana Mungu, wanasekula au watu wa uhuru na watu wanaoita katika shari, machafuko, tamasha na Tash ma Tash[1] ambao wanaomboleza hivi sasa kwa kuwa haipo tena.

Sehemu ya pili ni wale wanaoita katika kupetuka mipaka kwa mfumo kama wa Khawaarij na matendo ya wafuasi wao. Leo wendawazimu wametangaza, kwa madai yao, dola ya Kiislamu. Tunajua porojo hii tokea miaka ishirini ya nyuma. Wanampa kiapo cha utiifu na usikivu kiongozi wao kwa siri na kwa mfumo wao fasidi. Wote wana bay´ah zao za siri kwa mtu asiyejulikana. Hufanya hivo kila siku. Pale anapouawa tu anakuja Khaliyfah mpya. Hili liko karibu na al-Mahdiy wa Raafidhwah. Hivi sasa kumetangazwa Khaliyfah na ni kwa Waislamu wote. Kumetangazwa Khaliyfah wa Waislamu baada ya kuchinja na kufanya ya kufanya kwa ndugu wa Iraaq. Si yeye wala wale wapinzani wake katika Raafidhwah sio wazuri. Hakuna yeyote katika wao anayetakia kheri Ummah wa Kiislamu. Ni juu yetu kutahadhari pande zote mbili; yeye na wapinzani wake Raafidhwah. Wote wako katika shari. Wote ni wapotevu. Wote wanaweza kuwa na umoja wa kisiri dhidi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tahadhari na bay´ah hii ya kikhurafi na ya ki-Dajjaal. Wanamwita kuwa ni Khaliyfah wa Waislamu wa leo. Huyu ni Dajjaal na ni muongo anayeita katika upotevu. Amewaua Waislamu Syria. Hivi sasa amekuja kuwaua Waislamu huko Iraaq. Ameshirikiana na mjeuri wa Syria katika kuwaua Waislamu. Ndio maana mjeuri wa Syria amemuacha. Amemuacha kikamilifu. Hampigi vita kwa sababu anampa petroli kutoka Dayr-uz-Zawr.[2] Hivi sasa nguvu zote za shari za kimagharibi zimeshirikiana mgongoni. Nguvu hizi za shari ni zile zinazoitwa Khaliyfah wa Kiislamu, dola ya Raafidhwhah na zingine zote. Zote hizi zinashambulia Uislamu na Waislamu.

Tunamuomba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Anyanyue neno Lake, Ainusuru Dini Yake na Awavunje watu wa shari katika Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ na maadui wa Dini pasina kujali ni kina nani walio kati yao wanaotumbukia katika kupindukia au kuchuja. Ninawatahadharisha kuambatana na ma-Dajjaal hawa. Wakati walipotangaza nchi fulani kuna mmoja katika wafuasi wao amedai jinsi amevyomuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiashiria ni nani atayewaongoza katika Swalah na si yeye wala Jibriyl atayeongoza katika kiwanja fulani. Je, mnaona u-Dajjaal wanaodai? Ni juu ya Waislamu wawe hange.

Siku nyingine niliwanasihi ndugu Iraaq, kama jinsi nilivyowanasihi wengine katika nchi zingine, wabaki majumbani mwao. Wakivamiwa wajitetee:

“Mwenye kuuawa kwa ajili ya mali yake, heshima yake au uhai wake ni shahidi.”

Asipigane na kundi lolote lile katika haya. Yote yamo upotofuni; dola ya Raafidhwhah na dola inayoitwa ISIS. Wote hawa wako dhidi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Msijishughulishe nao. Hatuna lolote na wao. Tumuabudu Allaah, tujifunze na kuielewa Dini ya Allaah ili mwema aweze kustarehe au kustarehe kutokana na muovu.

—————–
(1) http://en.wikipedia.org/wiki/Tash_ma_Tash
(2) http://en.wikipedia.org/wiki/Deir_ez-Zor

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/varken-med-isis-eller-rafidhah/
  • Imechapishwa: 07/02/2017