Shiy´ah wa mwanzoni walikuwa wakiona kuwa Abu Bakr na ´Umar ndio wabora kuliko ´Aliy

Shiy´ah, wafuasi wa ´Aliy, walikuwa wakiona kwamba Abu Bakr na ´Umar ndio wabora kuliko yeye. Mvutano ulikuwepo tu kama yeye ni bora kuliko ´Uthmaan au hapana. Wakati huo hapakuwepo yeyote anayeitwa “Imaamiy” au “Raafidhwiy”. Mara ya kwanza kupata jina la “Raafidhwah” na wakawa Raafidhwah pindi Zayd bin ´Aliy bin al-Husayn alipojitokeza huko Kuufah katika ukhaliyfah wa Hishaam. Shiy´ah wakamuuliza kuhusu Abu Bakr na ´Umar ambapo akawatakia rehema. Wakamkataa. Ndipo akasema:

“Mmenikataa. Mmenikataa.”

Ndipo wakapewa jina la “Raafidhwah”, wakataaji.

Wengine wakachukua sehemu yake na wakaitwa “Zaydiyyah”, kwa sababu ya kujinasibisha naye. Tokea wakati huo Shiy´ah wakagawanyika kati ya Raafidhwah Imaamiyyah na Zaydiyyah. Kadri jinsi walivyozidi kuzama katika Bid´ah, ndivyo wakawa waovu zaidi. Zaydiyyah ni wajuzi, wakweli, wenye kuipa nyongo dunia na mashujaa zaidi kuliko Raafidhwah.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (2/96)
  • Imechapishwa: 15/12/2018