Shiy´ah hawana ´Aqiydah ya Ahl-ul-Bayt

Imaamiyyah wanakwenda kinyume na misingi mingi ya mafunzo ya Ahl-ul-Bayt wanayoamini. Hakuna yeyote katika maimamu wa Ahl-ul-Bayt kama mfano wa ´Aliy bin al-Hasan Abu Ja´far al-Baaqir na mtoto wake Ja´far bin Muhammad as-Swaadiq yeyote ambaye alikuwa akikanusha kuonekana kwa Allaah, akisema kwamba Qur-aan imeumbwa, akikanusha Qadar, akisema kwamba kuna andiko la wazi juu ya kwamba ´Aliy ndiye khaliyfah wa kwanza, mwenye kusema kwamba maimamu wamekingwa na kukosea au mwenye kumtukana Abu Bakr na ´Umar. Nukuu zilizothibiti na zilizopokelewa kwa njia nyingi kutoka kwa watu hawa zinatambulika vyema na ziko na wanazitegemea Ahl-us-Sunnah.

Mashaykh wa Raafidhwah wanakubali juu ya kwamba ´Aqiydah hii kuhusu Tawhiyd, sifa za Allaah na Qadar haikuchukuliwa si kutoka katika Qur-aan, Sunnah wala maimamu wa Ahl-ul-Bayt. Wanadai kwamba akili imefahamisha hivo, kama wanavosema Mu´tazilah. Uhakika wa mambo ni kwamba wameichukua ´Aqiydah yao kutoka kwa Mu´tazilah ambao ndio waalimu wao katika Tawhiyd na ´Adl. Wanakubali kwamba hakuna walichochukua kutoka kwa maimamu wa Ahl-ul-Bayt isipokuwa tu Shari´ah.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (2/368-369)
  • Imechapishwa: 11/12/2018