Shiy´ah al-Kishshiy anakiri myahudi ndiye muasisi wa pote

Baadhi ya wanachuoni wanataja kwamba ´Abdullaah bin Sabaa´ alikuwa myahudi ambaye aliingia katika Uislamu na akaonyesha mapenzi kwa ´Aliy. Katika uyahudi wake alikuwa akichupa mipaka juu ya Yuushu´ kwamba ndiye wasii wa Muusa. Baada ya kusilimu kwake akasema hayohayo baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya ´Aliy. Yeye ndiye wa mwanzo aliyetambulika kuzungumzia juu ya uongozi wa ´Aliy, kujitenga mbali na maadui wake, kuwashambulia wenye kumhalifu na kuwakufurisha.

  • Mhusika: Muhammad bin ´Umar al-Kishshiy (kfrk. 350)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ikhtiyaar Ma´rifat-ir-Rijaal (1/324)
  • Imechapishwa: 14/12/2018