Shirki ya al-Haakimiyyah inayong´ang´aniwa na wanaharakati

Miongoni mwa watu wako wenye kusema kwamba shirki ni kule kushirikisha katika Haakimiyyah, jambo ambalo kwa masikitiko makubwa linaonekana hii leo. Kuhukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah ni aina fulani ya shirki na inaitwa kuwa ni shirki ya utiifu. Hapana shaka kwamba kuwatii viumbe katika kuhalalisha yale aliyoharamisha Allaah au kuharamisha yale aliyohalalisha Allaah ni aina fulani ya shirki. Lakini kuna jambo ambalo ni kubwa zaidi kuliko hilo ambalo ni kumwabudu Allaah asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall) katika kuchinja, kuweka nadhiri, kutufu na kuomba msaada. Lililo la  wajibu ni kutahadharisha shirki yote na sio kuchukua sehemu yake na kuacha ambacho ni kikubwa na khatari zaidi kuliko. Shirki isifasiriwe kuwa ni shirki ya al-Haakimiyyah peke yake au shirki ya kisiasa na wanasema kuwa shirki ya makaburi ni shirki isiyokuwa na maana yoyote na kwamba ni nyepesi. Huku ni kuwa na ujasiri wa kipumbavu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Shirki ndio kubwa ambalo Allaah amekataza. Nayo ni kule kumuomba Allaah pamoja na wengine. Hii ndio shirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaath-il-Usuwl, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 29/03/2020