Shirki Haakimiyyah ni kubwa au ndogo?

Swali: Shirki Haakimiyyah ni kubwa au ndogo?

Jibu: Haya ni kutegemea na ufafanuzi kuhusu kuhukumu kinyume na Shari´ah. Wao wanasema kwamba haya ni miongoni mwa mambo ya kimatendo. Akiwa anaamini kwamba kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah inafaa na hakuna ubaya, kwamba ana khiyari kwa njia kwamba akitaka anaweza kuhukumu kwa yale aliyoteremsha au akaacha, hii ni kufuru kubwa inayomtoa katika Uislamu. Hapa hapana shaka. Haya ni kwa maafikiano. Ikiwa anaona kuwa kuhukumu kwa kanuni kunafaa,  kwamba ana khiyari kwa njia kwamba akitaka anaweza kuhukumu kwa yale aliyoteremsha au akaacha au baya zaidi akasema kwamba hizi sheria za wanaadamu ni bora kwa watu kuliko Qur-aan na ni bora kuliko hukumu ya Kiislamu, huu ndio ukafiri mkubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/01.mp3
  • Imechapishwa: 03/08/2018