Shikamana Na Waliokufa


Kanuni katika suala hili:

“Anayetaka kumfuata mtu basi afuate yule aliyekufa. Kwa sababu hakuna dhamana kuwa aliyehai hatosibiwa na fitina.”

Hakuna dhamana kuwa aliyehai hatosibiwa na fitina. Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufuatwa inakuwa wale waliokufa juu ya njia sahihi:

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ

“Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo uongofu wao.” (06:90)

Ama kuhusu wale waliohai, mpende mtu na msifu, lakini usimpe Tazkiyah kikamilifu. Kwa kuwa hujui ni hali ipi mtu atakhitimu nayo. Nyinyi wenyewe mnajua ni wangapi ambao wamesibiwa. al-Maghraawiy ameishia wapi? Abul-Hasan [al-Ma´ribiy] ameishia wapi? ´Aliy bin Hasan al-Halabiy ameishia wapi? Amekuwa miongoni mwa wanademokrasia. Hivi sasa tuko na al-Hajuuriy. Ameishia wapi? Ameungana nao. Wamekuwa hivi sasa ni wageni wake; Abul-Hasan, ´Aliy bin Hasan na watu hawa. Aliyehai hadhaminiwi kutojaribiwa.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://putselefa.com/jahja-al-hadzuri-je-zavrsio-sa-al-maribijem-i-al-halabijem/
  • Imechapishwa: 18/01/2017