Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya sherehe juu ya kumuaga kafiri kwa sababu ya kumaliza kazi yake? Ni ipi hukumu ya kumpa pole kafiri? Ni ipi hukumu ya kuhudhuria sherehe za makafiri?

Jibu: Swali hili lina mambo mengi:

La kwanza: Kufanya sherehe kwa ajili ya kumwaga kafiri. Hapana shaka kwamba huku ni kumuheshimisha au kuonyesha masikitiko kwa kutengana nae. Yote haya mawili ni haramu kwa muislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msianze kuwatolea salamu mayahudi wala manaswara. Pale mtapokutana nao katika njia basi walazimisheni kupita njia nyembamba.”

Mtu ambaye ni muumini wa kweli hawezi kumuheshimisha yeyote ambaye ni adui wa Allaah. Makafiri ni maadui wa Allaah kutokana na dalili ya Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ

“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake na Mitume Wake na Jibriyl na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.” (02:98)

La pili: Kumpa pole kafiri anapofiliwa na yule ndugu au rafiki. Wanachuoni wametofautiana katika hili. Kuna wanachuoni waliosema ya kwamba kuwapa pole ni haramu na kuna wengine waliosema kuwa inafaa. Kuna wanachuoni wengine wamepambanua zaidi na kusema ya kwamba ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa, kama vile kutarajiwa akasilimu au kujiepusha na shari yao ambayo hakuna namna ya kuiepuka isipokuwa kwa kuwapa pole, itakuwa inafaa. Vinginevyo itakuwa ni haramu.

Maoni yenye nguvu ni kwamba ikiwa katika kuwapa kwake pole kunafahamika kuwatukuza na kuwaheshimisha itakuwa ni haramu. Vinginevyo kutaangaliwa manufaa.

La tatu: Kuhudhuria sherehe zao na kushiriki katika furaha zao. Ikiwa ni sherehe za kidini, kama vile krismasi, basi kuhudhuria itakuwa ni haramu. Hili halina shaka. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Haijuzu kuhudhuria kwa makubaliano ya wanachuoni. Wanachuoni wameliweka wazi hilo katika wafuasi wa maimamu wa madhehebu mane kwenye vitabu vyao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/303-304)
  • Imechapishwa: 10/07/2017