Shaytwaan anampamba mwanamke wakati anapotoka nje


2688- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke ni uchi. Pindi anapotoka nje shaytwaan anampamba. Anakuwa karibu zaidi na Allaah wakati anapokuwa nyumbani kwake.”

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” (3036). Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh är autentisk na wapokezi wake wote ni waaminifu na wanaume wa Muslim mbali na al-Baghawiy. Ni mwaminifu kwa mujibu wa ad-Daaraqutniy.

Hapana shaka kwamba shaytwaan anampamba mwanamke hata kama atakuwa ni mwenye kufunika uso wake. Mwanamke ni uchi kwa hali zote pindi anapotoka nje. Hadiyth haina mahusiano yoyote na kwamba uso wa mwanamke ni uchi kwa maana ya ki-Fiqh. Wanachuoni wengi wanaona kuwa uso wa mwanamke sio uchi. Hayo yamebainishwa katika kitabu changu Jilbaab-ul-Mar´ah al-Muslimah”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/1/425)
  • Imechapishwa: 15/05/2019